Description
Mada hii inazunguzia mambo kumi amboyo yanamto mtu kati dini ya Uislam
بسم الله الرحمن الرحيم
MIONGONI MWA MAMBO AMBAYO YANAMTOA MUISLAM KATIKA UISLAM.
Imeandaliwa na kutafsiriwa na yunus kanuni Ngenda
Imepitiwa na abubakari Shabani.
Utangulizi:
Kila sifa njema zinamstahikia Allah Ambaye Ameumba kila kitu na akakitengeneza vizuri na kukipangilia, na akamfundisha adabu Nabii wetu Muhammad Rehma na Amani za Allah ziwe Juu Yake, kisha akazifanya kuwa ni nzuri zaidi,na akamteremshia Quraan ikiwa niuongofu kwa walimwengu,sala na amani ziwe juu yake na maswahaba zake na woote watakao mfuata kwa wema.
Uislam nidini ya kweli na ndio mfumo pekee wa maisha bora kwa mwanadamu,hivyo ikawa hakuna budi kuzungumzia mambo ambayo akiyafanya mwanadamu anatoka katika uislam hata kama yatabakia majina yake niyakiislam.
Yapo mambo mengi ambayo akiyafanya muislam anatoka katika uislam,miongoni mwa mambo hayo:
1-Ni kumshirikisha Allaah Aliyetukuka katika ibada.
Anasema Allaah:
(إِنَّ اللَّهَ لَا يَغْفِرُ أَنْ يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَنْ يَشَاءُ ۚ وَمَنْ يُشْرِكْ بِاللَّهِ فَقَدْ ضَلَّ (ضَلَالًا بَعِيدا
“Hakika Allaah hamsamehe mwenye kumshirikisha na Anasamehe yasiyokuwa hayo (ya shirki) kwa Amtakaye”
(An-Nisaa: 116)
Na Anasema Allah:
(..إِنَّهُ مَنْ يُشْرِكْ بِاللَّهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنْصَارٍ)
“Hakika mwenye kumshirikisha Allaah, (mtu huyo) Allaah Amemuharamishia pepo na mashukio yake ni motoni na madhalimu hawana mwenye kuwanusuru”
(Al-Maaidah: 72)
na miongoni mwa hizo shirki ni kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah, kama anayechinja kwa ajili ya majini au makaburi.
2-Mwenye kufanya (kuweka) baina yake na Allaah viunganishi akawa anaviomba viunganishi hivyo na kuvitaka uombezi na kuvitegemea, basi hakika mtu huyo amekufuru kwa makubaliano ya wanavyuoni.
3-Asiyewakufurisha washirikina au akawa ana shaka katika ukafiri wao au akaupitisha (akausahihisha ) ukafiri wao amekufuru.
4-Mwenye kuamini kwamba muongozo wa asiye kuwa Mtume Muhammad (S.a.w) ndio muongozo ulio kamili kuliko muongozo wa Mtume, au ya kwamba hukmu ya mwengine ni bora kuliko hukmu yake Mtume (S.a.w), kama yule anayefadhilisha hukmu za Matwaghuut kuliko hukmu yake Mtume (S.a.w) basi mtu huyo ni kafiri.
5-Mwenye kuchukia chochote katika aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekufuru.
6-Mwenye kufanyia mzaha (shere) kwa chochote katika dini (Uislam) au akafanya utani katika thawabu au katika adhabu za Allaah (S.w) amekufuru.
Na dalili ni neno Lake Allaah:
. لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُمْ بَعْدَ إِيمَانِكُمْ قُلْ أَبِاللَّهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنْتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ،
“Sema: Je, kwa Allaah na Ayah Zake na Mtume wake ndio mukizifanyia mchezo, (na mzaha?) musitoe udhuru hakika mumekufuru baada ya kuamini.” (At-Tawbah: 65-66)
7-Uchawi: na miongoni mwa huo uchawi ni uchawi wa kutenganisha na kupendanisha basi yeyote mwenye kufanya huo uchawi au akauridhia! Amekufuru.
Anasema Allah:
َ(..وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَا إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُرْ ۖ
“Na hawakuwa wakimfundisha huo uchawi yeyote mpaka wamwambie hakika sisi ni mtihani basi usikufuru.
(Al-Baqarah: 102)
8-Kusaidiana na kuwa pamoja na washirikina dhidi ya Waislamu, na dalili ni kauli ya Allah:
(..وَمَنْ يَتَوَلَّهُمْ مِنْكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ ۗ إِنَّ اللَّهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ)
“Na atakaye wapenda makafiri (na kuwafanya ni wasiri wao) katika nyinyi basi hakika yeye ni katika wao. Hakika Allaah Hawaongozi madhalimu.” (Al-Maaidah: 51)
9-Mwenye kuamini ya kwamba baadhi ya watu wanaweza kutoka katika shari’ah ya Mtume Muhammad (S.a.w) kama vile alivyoweza kutoka Al-Khidhr katika shari’ah ya Muusa, basi mtu hiyo ni kafiri.
10-Kuikataa na kuipa mgongo dini ya Allaah (S.w) na akawa hajifunzi chochote katika dini.
Na dalili ni neno Lake
(وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنْ ذُكِّرَ بِآيَاتِ رَبِّهِ ثُمَّ أَعْرَضَ عَنْهَا ۚ إِنَّا مِنَ الْمُجْرِمِينَ مُنْتَقِمُونَ)
“Na ni nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyekumbushwa Aayah za Mola wake kisha akazikataa,Hakika Sisi ni wenye kuchukua kisasi kwa watu wabaya.
(As-Sajdah: 22)
Na wala hakuna tofauti mambo haya yanayomtoa Muislamu katika Uislamu kwa yule anayefanya utani au anayefanya kweli au anayeogopa, isipokua anayetenzwa nguvu (kama kushikiwa silaha na akalazimishwa kufanya hayo). Na yote hayo tuliyoyataja ni katika mambo makubwa yanayohatarisha sana.
Ndugu katika imani tumechukua fursa hii ya kukumbushana kwasababu mambo haya yanafanyika sana katika jamii zetu, kwa hivyo yapaswa kwa Muislam mwenye imani ya kwamba kesho (Qiyama) atasimaishwa mbele ya Allah na kuulizwa juu ya kila jambo! Basi ajihadhari na mambo haya na ayaogope kwa nafsi yake.
Tunajilinda kwa Allaah na mambo yanayopelekea hasira zake na adhabu Zake kali, na rehma na amani zimfikie kiumbe bora Mtume wetu Muhammad (S.a.w) na jamaa zake na Maswahaba wake wote.