×
New!

Bayan Al Islam Encyclopedia Mobile Application

Get it now!

SIFA ZA UDHU WA MTUME (S.A.W) (Kiswahili)

Maandalizi: Fahad Bin Abdurahman Al Shuwaybu

Description

Mada hii inazunguzia namna alivyotawadha Mtume wetu Muhammad (S.a.w)

Download Book

    بسم الله الرحمن الرحيم

    NAMNA ALIVYO TAWADHA NABII MUHAMMAD SWALLA LLAHU ALAYHI WASALLAM

    MTUNZI NI SHEKH:

    FAHDI BIN ABDURRAHMAN ASSHUWAYYIB

    IMETAFSIRIWA NA SHEKH:

    YASSINI TWAHA HASSANI

    IMEPITIWA NA SHEKH:

    ABUBAKARI SHABANI RUKONKWA

    UTANGULIZI

    Baada yakumshukuru Mwenyezi Mungu nakumtakia rehma na amani Mtume Muhammad swalla llahu alayhi wasallam pamoja na ahli zake na maswahaba zake na waislamu woote watakao fuata mwenendo wake mpaka siku ya qiyama. Tuna muomba Mwenyezi Mungu atujaalie nasi pamoja na wazazi wetu na wake zetu na watoto zetu na mashekhe zetu tuwe miongoni mwa hao. (AMIN).

    AMMABAAD: Hakika mazungumzo bora ni maneno ya Allah' na muongozo ulio bara zaidi ni muongozo wa Mtume Muhammad swalla llahu alayhi wasallam' namambo mabaya ndani ya dini niyale yakuzushwa' nakila uzushi ni bidaa' nakila bidaa ni upotovu' nakila upotovu humpeleka mtu motoni. Mwenyezi Mungu atuepushe na moto wa jahannam. (AMIN).

    Ndugu zangu makala hii inazungumzia Ubora wa Udhu na namna alivyo kua akitawadha Mtume wetu Muhammad swalla llahu alayhi wasallam na hadithi zote kuanzia mwanzo mpaka mwisho zitakua ni sahihi tupu' kwa mapenzi yake Allah. Napakiwepo tofauti kati ya wana chuoni kwenye maswala yeyote tutaeleza kauli yenyenguvu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atujaalie tuwe tuna tawadha Kama alivyo tawadha Mtume wetu Muhammad swalla llahu alayhi wasallam. (AMIN).

    قَال رَسُولُ اللهِ صلَّى اللهُ عَليهِ وسلَّم: "مَن تَوضَّأ هكذا غُفِرَ لَه مَا تَقدَم مِن ذَنبهِ وَكَانت صَلَاته وَمشيُه إلى المَسجد نافِلة" رواه مسلم.

    Amesema Mtume Muhammad swalla llahu alayhi wasallam: {Yeyote atakae tawadha hivii! husamehewa madhambi yake yalio tangulia' na itakuwa swala yake na kwenda kwake muskitini hupata malipo ya ibada za sunna}. kaipokea Hadithi hii Imam Muslim.

    MAANA YA KUTAWADHA:

    Kutawadha maana yake nikutumia maji yalio kua safi katika viungo maalum alivyo vibainisha Mwenyezi Mungu ndani ya Qur'ani na akavifafanua Mtume Muhammad ndani ya hadithi zake sahihi.

    USHAHIDI WA KUTAWADHA NDANI YA QUR'ANI NA SUNNA:

    قَالَ اللهُ تَعَالى:}يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْن{المائدة /6

    Amesema Mwenyezi Mungu Mukufu:

    1- kutoka kwa abii hurayra radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: {Hakubali Mwenyezi Mungu swala ya mmoja wenu anapo huduthi (anapokua hana udhu) mpaka atawadhe}. Kaipokea imam Bukhari (6954) na imam Muslim (225) na wengineo.

    2- kutoka kwa Abdullah bin omar radhi za Allah ziwe juu yao amesema: nilimsikia Mtume Muhammad swalla llahu alayhi wasa llam akisema: {Hakubali Mwenyezi Mungu swala bila ya twahara; na sadaka ilio patikana katika njia ya khiyana au wizi}. Kaipokea imam Muslim (1/160) na wengineo.

    3- kutoka kwa Abdullah bin abbasi radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: {kwa hakika nimeamrishwa kutawadha pindi nnapo taka kutawadha}. Kaipokea imam abuudaudi na tirmidhi na annasaai. angalia kitabu swahihil-jaamia (2337).

    4- kutoka kwa abii saidi al-khudriy radhi za Allah ziwe juu yake: kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: {ufunguo wa swala ni twahara……..}. Kaipokea imam abuudaudi na tirmidhi na ibnu maajah. angalia swahihil-jaamia (5761).

    FADHILA ZA KUTAWADHA:

    5- kutoka kwa abii hurayra radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: {Jee! Nikwaambieni mambo ambayo mkiyafanya Mwenyezi Mungu atakufutieni madhambi yenu na kukupandisheni daraja? Maswahaba wakasema ndio ewe mtume wa Allah! Akasema: kutawadha vizuri wakati wa baridi na hatua zinapo kua nyingi wakati wa kwenda muskitini na kusubiria swala baada ya kumalizika swala huko ndiko kuizuia nafsi katika kheri}.

    Kaipokea imam Muslim (1/151) na wengineo.

    6- kutoka kwa abii hurayra radhi za Allah ziwe juu yake kwamba: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: {atapo tawadha mja muislamu – muumini akaosha uso wake' huondoka madhambi yote ambayo yamepatikana kwa sababu ya macho' kwa maji aliyo weko usoni au kwa tone la mwisho litalo dondoka kutoka usoni! Atapo osha mikono yake huondoka madhambi yote ambayo yamepatikana kwa sababu ya kufanywa na mikono! kwa maji aliyo weko mikonoi au kwa tone la mwisho litalo dondoka kutoka mikononi! Atapo osha miguu yake huondoka madhambi yote ambayo yamepatikana kwa sababu ya kutembea miguu yake! kwa maji aliyo weko miguuni au kwa tone la mwisho litalo dondoka kutoka miguuni mwake! Mpaka anamaliza kutawadha akiwa msafi hana dhambi!}.

    Kaipokea imam Muslim (1/148) na wengineo.

    7- kutoka kwa abii hurayra radhi za Allah ziwe juu yake kwamba: Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alienda makaburini akasema: {amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yenu nyinyi mlio lala kwenye nyumba hizi! Na sisi akipenda Mwenyezi Mungu tutakutana nanyi' natamani lau kama tungeli kutana nandugu zetu! Maswahaba wakasema: ewe Mtume wa Mungu sisi sio ndugu zako? Akasema: nyinyi ni maswahaba zangu! Nandugu zetu niwale ambao bado hawajaja! Maswahaba wakasema: ewe Mtume wa Mungu utawajuaje watu ambao hawajaja katika umati wako? Akasema: niambieni lau kama kunamtu yupo na farasi warangi nyeupe kachanganyikana na farasi wa rangi nyeusi na weupo usoni mwake hawezi kumtambua farasi wake warangi nyyyeupe? Maswahaba wakasema ndio anaweza kutmbua farasi wake ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu' akasema Mtume rehma na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: kwa hakika hao ndugu zangu watakuja siku ya qiyama wakiwa na alama nyeupe sehemu za udhu! Na mimi ntawatangulia kwenye khodi langu (birika) }

    عَلَى الْحَوْضِ أَلاَ لَيُذَادَنَّ رِجَالٌ عَنْ حَوْضِى كَمَا يُذَادُ الْبَعِيرُ الضَّالُّ أُنَادِيهِمْ أَلاَ هَلُمَّ. فَيُقَالُ إِنَّهُمْ قَدْ بَدَّلُوا بَعْدَكَ. فَأَقُولُ سُحْقًا سُحْقًا{.مسلم.

    8- kutoka kwa Abii Umaama radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: {Atapo tawadha Muislamu hutoka Madhambi yake kupitia masikio yake na macho yake na mikono yake na miguu yake' anapo kaa kwaajili ya swala hukaa huku kasamehewa madhambi yake}. Angalia swahihil-jaamia (448).

    9- kutoka kwa Abii Malikil-ash-ary radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: {kujitwaharisha ni nusu ya iimani' na kusema: Al-hamdu lillahi hujaaza miizani' au hujaza baina ya mbingu na adhi' na swala ni nuuru' na sadaka nimtetezi' na subira ni muangaza' na qur-ani nihoja kwako au juu yako! Watu wanapo toka asubuhi majumbani wanakua wamegawanyika katika sehemu mbili: kuna ambao wanazitoa nafsi zao katika kumtii Mwenyezi Mungu' wengine katika kumuudhi Mwenyezi Mungu!}. Kapokea imam Muslim (1/140) na wengineo.

    10- kutoka kwa Othman bin Affan radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: {yeyote atakae tawadha na akafanya vizuri katika udhu wake! Huondoka madhambi yake kutoka katika mwili wake mpaka yanapenya chini ya kucha zake!}. Kapokea imam Muslim (1/140) na wengineo.

    11- kutoka kwa Othman bin Affan radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: {Yeyote atakae tawadha hivii! husamehewa madhambi yake yalio tangulia' na itakuwa swala yake na kwenda kwake muskitini hupata malipo ya ibada za sunna}. kapokea Hadithi hii Imam Muslim. {3/113}.

    12- kutoka kwa Abdullah bin Omar radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: {atapo tawadha mmoja wenu aka kamilisha udhu wake' kisha akatoka kuelekea muskitini' hakuna kilicho mtoa nyumbani kwake zaidi ya swala hautoacha mguu wake wakushoto kufutas dhambi na huandikwa mema kwa mguu wake wa kulia mpaka atapo ingia muskitini! Laiti wangelijua watu faida inayo patikana katika swala ya ishaa na alfajiri wangeli ziendea hizo swala mbili japo kwa kutambaa}. kapokea Hadithi hii Twabrani.

    Angalia swahihil-jaamia (454).

    13- kutoka kwa abii hurayra radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: {yeyote atakae tawadha' aka kamilisha udhu' kisha kenda muskitini kawakuta watu wamekwisha maliza kuswali' humpa Mwenyezi Mungu malipo ya wale woote walio swali swala hiyo na walio hudhuria bila kupunguziwa chochote katika malipo yao}. Kaipokea imam abuudaudi na annasaai na wengineo. angalia kitabu swahihil-jaamia (6039).

    14- kutoka kwa zaidi bin Khalid al-juhany radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake Alisema: { yeyote atakae tawadha' aka kamilisha udhu' kisha akaswali rakaa mbili hakuizungumzisha nafsi yake mambo ya kidunia Mwenyezi Mungu humsamehe madhambi yake yalio tangulia}. Kaipokea imam abuudaudi na wengineo. angalia kitabu swahihil-jaamia (6041).

    15- kutoka kwa Uqba bin Aamir radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: { yeyote atakae tawadha' aka kamilisha udhu' kisha akaswali rakaa mbili kwa unyenyekevu wa nafsi na kiwiliwili nijuuyake mtu huho kupata pepo!}. Kaipokea imam nnasaai. angalia kitabu swahihil-jaamia (6062).

    16- kutoka kwa Othman bin Affan radhi za Allah ziwe juu yake amesema' nilimsikia Mtume Muhammad swalla llahu alayhi wasa llam akisema:{yeyoto atakae tawadha kwaajili ya swala na aka kamilisha udhu' kisha kaelekea muskitini kwaajili ya swala ya faradhi' akaswali pamoja na watu au pamoja na jamaa au muskitini Mwenyezi Mungu humsamehe madhambi yake!}. kaipokea Imam Muslim {1/144} na wengineo.

    17- kutoka kwa Ally radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake Alisema: {kukamilisha udhu wakati wa baridi kali' na hatua zikiwa nyingi kuelekea muskitini na kusubiria swala baada ya swala' huondoa madhambi}. kaipokea Imam Hakim {1/132} na wengineo.

    معلومات المادة باللغة العربية